Ni masaa machache tu ndiyo yamebaki ili watu wa Sudan kusini wapige kura ya maoni itakayoleta uhuru kwa watu.
Twasema Kaskazini mwa sudan, "ubaki na ugoigoi wako." Sheria yenu iwe
ugombezi wenu. Akilini mwetu kwa nusu ya karne hapa kusini, tuliona dunia
ikiwayawaya nu kuyugayuga tukitafuta usaidizi wa kila aina ili tupate haki
zetu. Mpira wakati huu uko kwa koti yenu.
Mwayowayo na mkipenda
mlia machozi. Mola ni wa kila binadamu naye ni mwenye haki na upendo.
Kwaherini. Na msisahau kwamba tutatengana na kufarakana nanyi milele kwa
sababu tuliumia sana mikononi mwenu.
Katika vita vya
kupigania uhuru, vita ambavyo wataalamu huwaamini ni ndefu barani Afrika,
tulikufa kwa risasi, wanyama wa msitu na wa pori walipata chemsha kinywa na
miili wetu, wanawake wetu walinajisiwa, wengi wetu walichochewa na kufukuzwa
nchini mpaka wakapata makao wa ghafula ughaibuni, tulichekeshwa tukiwa
tunajaribu kutulia ugenini, watoto wetu wamezaliwa nje ya nchi hata hawajui
Sudan ni upande gani wa dunia, kila kitu kimegeuka na kutugeukia vibaya mpaka akili zetu kwa sababu ya uhayawani wa wachache huku Sudan.
Lakini sasa, ijapo
tulidhani Mungu hasikii, tunampatia shukrani, tunamwabudu na kumheshimu kwa
kuwa mwishowe, anaonekana kama husikia watu wake, duniani kote na hususan,
watu wake Kusini mwa Sudan.